Awanguapo halezi! anagaotea na kuta, 
Wanawe humpa kozi na mwewe akakamata. 
Wakashilia kwa njozi na mwivi nae kapata 
K’uk’u wa mkata k’ata na akita haangui. 
 
Hapokewi masikini; mambo yakwe yana k’ota 
Milele hushuka tini, heshi ndaa, wala nyota! 
Mkiwa hana mwandani, ha ndugu kufuata 
K’uk’u wa mkata k’ata na akita haangui. 

*

Muyaka bin Haji al Ghassany (1776 – 1840) was a famous poet of Mombasa.